Sunday, 25 November 2018

Barua ya wazi kwa Rais Uhuru Kenyatta

ad300
Advertisement

Rais Uhuru akihutubia wakati moja.
MOHAMMED HATIB ABDALLAH
|| Email: muhammadabdallah944@gmail.com

25th November, 2018

Kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya
Uhuru Muigai Kenyatta,

S.L.P - 80100,
Ikulu ya Nairobi,

Mtukufu Rais,

                               MINT: MKOMBOZI WA WALALA HOI KENYA

Rais, Natumai ubuheri wa afya kwa sasa hapo ulipo.
Baada ya kukuona uko mchangamfu katika hafla kadhaa ulipozuru eneo hili la kaunti ya Mombasa ukiwa bega kwa bega na Gavana wa Kaunti ya Mombasa na magavana wengine wa kaunti za hapa mkoani Pwani katika kuanzisha na kufungua miradi kadhaa itakayo wanufanisha wakaazi wa mkoa wa Pwani na Kenya kwa ujumla.
Lakini leo Bwana Rais kwa niaba ya wakenya walalahoi nimeamua kukuandikia waraka huu kukuomba uyatilie mkazo maswala haya kwa niaba ya wakenya wa tabaka la chini.
La kwanza nililolipa kipao mbele ni swala la reli ya kisasa ya SGR kwa sababu wakenya wengi wamepoteza ajira baada ya shirika la reli nchini kuanzisha safari za kubeba makasha kutoka bandari za Mombasa.,wakenya waliokuwa wakitegemea kubeba makasha hayo kupitia malori yao wingi sasa wamebaki wakilia hali huku uchumi mzito ukizidi kuwalemea .
Ulipofungua mradi wa SGR wakenya wengi walifurahia lakini athari zake sasa zimeanza kujitokeza sio kwa madereva tu bali hata kwa wenye mahoteli na wenye vyumba vya wageni katika barabara kuu ya Mombasa Nairobi bila kuwasahau wafanya biashara wanaofanya biashara kando kando na barabara hii .
Rais ombi langu kwa niaba ya wakenya kwako kupitia kwa shirika la reli nchini na kwa waziri wa uchukuzi wapunguze au wagawiyane makasha na madereva wa malori ili hali ya maisha yao na ya hawa wanabiashara irudi kama mwanzo.
Pili Rais ni swala la mnyonge azidi kuwa mnyonge kwa mzigo wa serikali , ni hivi majuzi tu wabunge na maseneta walieka tofauti zao za vyama na wakaja pamoja na kuungana mkono kupitisha mswaada wa nyongeza za mishahara na marupurupu huku wakenya wakawaida wakizidi kuemezewa mzigo huu.
Rais kumbuka kiongozi bora hujulikana wakati wa matatizo na shida kwa heshima na taadhima Rais simama imara katika kumkomboa mkenya huyu mlalahoi kutoka kwa midomo ya viongozi wasio na utu wala huruma kwa wakenya hivyo basi ifikiapo tarehe 27 mwezi Novemba mwaka 2018 usitie sahii mswaada huu kwani wakenya watazidi kuwa katika hali ngumu kimaisha na kiuchumi .
Kumalizia Rais ni swala la Blue Economy ulipofungua warsha juzi katika hoteli ya pride inn katika kaunti za Mombasa ambayo ilileta pamoja magavana wote wa kaunti zote sita za pwani wapwani tulifurahia na kupokea mradi huu kwa mikono miwili kikunjufu huku tukitarajia mengi mazuri kutoka kwa mradi huu, ombi langu kwako mtukufu Rais ni kuwa mradi huu unufaishe wakenya wa tabaka la chini wala sio wale watabaka la walio wachache nchini. Ni mradi najua utakao zalisha ajira hivyo basi kama katika katiba yetu ya Kenya naomba zile asilimia zilizotengwa ziwanufaishe watu wa eneo husika wala isiwe kama swala la Bandari kuwa na wingi wa wafanyakazi kutoka eneo flani au mradi ule wa Base Titanium ambapo umeawacha wakaazi wa kaunti ya Kwale wakilia ngoa nao.
Kukuandikia barua sio kukukejeli wala kukukosoa lakini fahamu anayekwambia uendako kuna shimo hakunyimi safari ila anakujali.
Nina mengi ya kukueleza lakini mdaa haunirusu kumbuka Kenya ni jina nchi ni sisi wanainchi .
Jina langu ni Mohammed Hatib mwandishi wa habari katika stesheni ya Radio Salaam Mombasa,
Shukrani.
 

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: