Advertisement |
Mgonjwa huyo anaugua maradhi ya saratani ya njia ya uzazi na angestahili kuondoka hospitalini humo siku ya Ijumaa, Julai 20 kama angekuwa amelipa kikamilifu salio. “Tunamsubiri mumewe au mbunge aliyemleta hapa kuja kulipa bili hiyo. Hatuwezi kumruhusu kuondoka pasipo idhini kutoka kwa wakuu wetu,” duru kutoka hospitali hiyo zilisema. Mgonjwa huyo, kulingana na duru hospitalini humo vilevile alikuwa na tatizo sugu la upungufu wa damu, hospitali hiyo haikuwa na damu inayolandana ya kumweka. Baadaye alifanyiwa upasuaji.
Kulingana na Karisa Kahindi, mumewe mwanamke huyo yuko tayari kumsaidia lakini changamoto za kiuchumi zimemlemea. “Niko radhi kusaidia lakini kutokana na changamoto za kifedha na kwamba nina mke wa pili na watoto kadha, siwezi,” alisema. Isitoshe, mume huyo alisema kabla ya mkewe kulazwa hospitalini, hakufahamishwa kwa sababu mwanamke huyo alikuwa akiishi na wazazi wake hadi kufikia sasa. Juhudi za kumfikia mbunge ili kusikia upande wake ziliambulia patupu huku msaidizi wake akisema hajakuwa akijihisi vyema kwa juma moja.
0 comments: