Tuesday, 15 May 2018

MESSI KIDEDEA KWA MAGOLI UROPA

ad300
Advertisement
Lionel Messi anatazamiwa kupokea tuzo la mfungaji bora uropa baada ya Salah kukamilisha msimu kwa magoli 32 .
Mabao hayo 32 yalitosha kumwezesha raia huyo wa Misri kuweka rekodi mpya ya Ligi Kuu ya Uingereza
 Mohamed Salah alikuwa ametarajiwa mno kulitwaa tuzo la mfungaji bora uropa wakati alipopiga mechi yake ya 38 ya Ligi Kuu ya Uingereza, lakini hilo halikutokea huku goli la Salah kwenye mechi yao ya mwisho wa msimu dhidi ya Brighton, ilimwezesha tu kupata jumla ya mabao 32. Hata hivyo, alikosea mabao mawili ili kumkaba Lionel Messi ambaye alikuwa na magoli 34 kwenye  Ligi ya La Liga huku akiwa bado ana mechi moja ya kucheza. Ciro Immobile wa Lazio anaongoza kwa ufungaji katika ligi ya Serie A kwa magoli 29 na ana mechi moja ya kucheza kabla ya kuufunga msimu nyumbani dhidi ya Inter Milan wikendi hii nayeye atahitaji zaidi ya mujiza kumpiku Messi. Ikiwa mambo yatabakia yalivyo sasa, Harry Kane atamaliza katika nafsi ya tatu kwa magoli 30 huku, Robert Lewandowski akifuata kwa magoli 29.  ni wachezaji wawili zaidi ya Messi ama Ronaldo walio wahii kuchukua tuzo hiyo. Diego Forlan wa Atletico Madrid alifunga mabao 32 mwaka wa 2009, na kuchukua tuzo hiyo huku Suarez akilitwa 2016 akiwa na Barcelona na kugawana na Ronaldo baada ya kupachika kimyani magoli 31 akiwa na Liverpool mnamo mwaka wa 2014. 
Orodha ya wafungaji Bora 
1. Lionel Messi, Barcelona — 34
2. Mohames Salah, Liverpool — 32
3. Harry Kane, Tottenham — 30 
4. Robert Lewandowski, Bayern Munich — 29
5. Ciro Immobile, Lazio — 29
6. Edinson Cavani, PSG — 28
7. Mauro Icardi, Inter — 28
8. Cristiano Ronaldo, Real Madrid — 25
9. Jonas, Benfica — 33
10. Luis Suarez, Barcelona — 24
Mohamed Salah wa Liverpool alitajwa mshindi wa tuzo hiyo wa Ligi Kuu ya Uingereza 2017 – 2018 kwa magoli 32 kwenye klabu Mchezaji huyo wa umri wa miaka ishirini na mitano alitajwa kuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli 32 katika msimu mmoja wa EPL na hii ni baada ya kuifungia Reds 4-0 dhidi ya Brighton & Hove Albion katika uga wa Anfield Jumapili, Mei 13.

 Alan Shearer aliiweka rekodi hiyo 1996 kwa kufunga magoli 31, lakini Cristiano Ronaldo na Luis Suarez wakaichukua 2008 na 2014 mtawalia .
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: