Monday, 11 September 2017

LADHA YA MZIKI WA PWANI

ad300
Advertisement
Kwa sasa katika mitandao ya kijamii tunakutana na habari za wasanii wawili wa Tanzania tunazugumzia Ali Kiba na Diamond wa lebo ya Wasafi kwa sasa wameteka tasnia nzima ya usanii  na soko la mziki kwa ujumla sio Tanzania tu bali hata Kenya na Afrika Mashariki kiujumla.
Swali linakuja ladha ya mziki wa Pwani iko wapi ? tatizo ni nini kwa ujumla , je ni mashabiki wa mziki au ni wasanii wenyewe ndio wanafanya tasnia hii kuwa haina dhamani .
Wako wapi wasanii kama Kaa la Moto , Fat-S,Dazlah,Rojo-Mo,Totii,Dogo Richy,Escobar,Chapatizo,Ally B , Cannibal,Susumila,Chikuzee,Nyota Ndogo na wengi wengineo ile ladha ya miaka ya nyuma imepotelea wapi? watu na viatu , ziki la nazi na vibao vingine mbona hatuzioni tena .
Wasanii wa tanzania wana kipi ambacho wasanii wetu wa pwani hawana , je ni ubunifu au ni kutojali kazi ya usanii?
Wasanii kama Diamond na Ali Kiba kwanini wanazidi kupata umaarufu kila kukicha na wasanii wetu bado wako chini tu .
Inasikitisha sana kuona jamii imetekwa nyara na wasanii wa nchi za nje kama tanzania , nigeria na kwingineko ilihali hawana habari na wasanii wa pwani na hata ukiwa umepanda matatu utaona ngoma zinazoekwa nyingi ni za nje sio za hapa pwani.
Tatizo kubwa haswa ni nini ndio swali ambalo kila mmoja wetu ajiulize kuhusu hii tasnia ambayo wasanii wengi wamejipatia umaarufu na kuwa matajiri .
Je nani amezembea mahali ni msanii  au shabiki au mshaka dau kwenye tasnia ya mziki au ni mapromota bado hawajafanya kazi ya ziada kuhakikisha wasanii wanapata umaarufu kama ule wa wenzao wa nje hii inapelekea wasanii wanaokuja kwa kasi kuvunjika moyo mapema kama vile msanii wa hip pop kwa jina Monsta kina Brbya na wengineo wengi kwani mpaka sasa kazi zao sio kila mtu anazijua hapa pwani .
Wasanii wa Tanzania na Afrika Mashariki wingi wao kando na mziki wanajishuhulisha na mambo mengine kujikuza na kujipa umaarufu zaidi kwa mfano kwa sasa tuko na njugu zinazoitwa diamondkaranga ambazo msanii Diamond anajipatia kipato kupitia biashara hiyo.
Wananchi wengi niliowahoji wana uliza wasanii wa pwani mko wapi mbona mnachukua mda mrefu kuachilia vibao pia wanawataka wazidii kukaza kamba katika tasnia hii na warudishe hadhi ya mziki wa pwani pale ilipokuwa pia waandaaji wa matamasha wazidi kuanda matamasha zaidi ilikuwapa fursa wasanii kuj
iuza ndani na nje ya Pwani kama lile la Fiesta ambalo huleta wasanii wa Tanzania pamoja kuzunguka Tanzania nzima wakiwatumbuiza mashabiki wao, kwanini hapa pwani halifanyiki?
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: