Advertisement |
Hii ni baada ya Mahakama ya juu kufutilia mbali ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta na kuamuru tume ya uchaguzi ya IEBC kuandaa uchaguzi mpya ndani ya siku 60.
Sasa mawakili wamaswala ya katiba wanasema kuwa kuna uwezekano wa mkondo wa tatu wa urais, ikizingatiwa mkabano wa koo baina ya kinara muungano wa NASA Raila Odinga na Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee, kwani hakuna uwezekano wa mshindi kwenye raundi ya kwanza.
Wataalamu hao wanasema kwamba ikiwa hakutapatikana mshindi atakaejizolea asilimia hamsini na kura moja zitakazo pigwa, itabidi taifa kuregea kwenye debe kutafuta atakaye iongoza nchi kwa mara ya tatu,kwani uchaguzi huu utachukuliwa kuwa wa kwanza.
Alisema wakili Gordon Ogolla kuwa uchaguzi tunaoenda kushiriki ni wa kwanza kwani ni agosti 8 ulifutiliwa mbali kumaanisha hauhisabiwi kikatiba.
0 comments: