Tuesday, 19 September 2017

MONSTA GUMZO MTAANI

ad300
Advertisement

Katika pita pita zangu za kusaka habari ilinikuhabarishe,nilifanikiwa kufika katika mji  wa kitalii wa Watamu na kubahatika kupatana na mwanamziki anayekuja kwa kasi Monsta.
Monsta ni nani haswa.
Monsta, ambaye kwa majina kamili anaitwa Furaha Simon, ni kijana aliye na umri wa miaka 27 aliye na makazi yake katika mji wa Watamu katika mtaa wa Timboni au Kidogobasi, Furaha ambaye jina la usanii mashabiki wanamuita Monsta ni mtoto wa pili wa mwisho katika familia ya watoto sita.
Alianza kuimba akiwa shule ya msingi. Aliimba miondoko ya ragga ambako alianzisha kundi la wasanii wenzake waliojitaa 24 na kufanikiwa kuandika wimbo wa kwanza ikienda kwa jina la sauti ya machizi ambayo haikufanikiwa kwenda hewani.
Monsta alipomaliza kusoma shule ya msingi ambako alikuwa mwanafunzi bora kwenye kata ya Watamu kwenye mitihani wa kitaifa wa Kcpe alifanikiwa kujiunga na shule ya upili ya Kenyatta iliyoko Mwatate katika kaunti ya Taita Taveta, ambako alianzisha kundi la kucheza haswa kwenye shughuli za masomo ambako ndoto ya kuwa mwananziki ilizidi kupata ari na kugundua kipaji kingine cha kurap.

Hapo ndipo alipoanza kuandika nyimbo ambazo zilieleza zaidi matatizo ambayo yanawakumba wanafunzi wenzake shuleni, aliendelea hivo mpaka alipofukuzwa kutokana na misimamo mikali hapo shuleni.
Alijiunga na shule ya Mombasa Baptist iliyoko katka kaunti ya Mombasa alipofanya mtihani wa kitaifa wa KCSE katika shule hiyo .
Mwaka wa 2013 alijiunga na shirika lisilo la kiserekali la elimu lililo na makao yake katika mji wa Watamu la Aiducation International Kenya ambako alifanikiwa kupelekwa kuwa mwalimu wa shule ya upili katika shule ya upili ya Kavunyalalo akitumikia tarajali (internship).
Akiwa mwalimu wa shule ya upili alifanikiwa kuwa balozi wa mazingira,alifanikiwa kupanda miti isiyohesabika kuokoa mti wa mkoko katika bahari ya mji huo
Mwaka uliofuata alifanikiwa kuwa balozi wa kupambana na mdudu funza katika shule zilizoko eneo hilo huku akiendelea na kazi yake ya kuwa msanii wa kuimba miondoko ya rap. 

Kando na kazi ya mziki, Monsta pia ni mchezaji mzuri wa mpira wa kikapu,mazoezi ya viungo na mneguaji wa viungo mzuri .
Pia amekuwa kielelezo kizuri kwa jamii kwa kuwa msanii wa kwanza katika mji huo kuanzisha biashara yake mwenyewe inayo msaidia kimapato haswa kurekodi nyimbo, Monsta anauza shati za kijanja bila kusahau kofia za kijanja ambako bei zake hazifananishwi na bei za maduka ya jumla haswa kwa vijana wa kileo .
Katika safari yake ya mziki, alianza kurekodi nyimbo zake akiwa nyumbani kwao kupitia kinasa sauti cha binamu yake ambaye alikuwa mwanafunzi wa masomo ya uanahabari.
Monsta ametoa vibao kadhaa kwa sasa vinavyo sikika hewani na kuzidi kupendwa na jamii kama vile Vasco da Gamma , Deliver na vingi vingenevyo .
Kwa sasa kwenye runinga zetu anazidii kushika mitandao ya kijamii na kuorodheshwa kwenye maredio kwa kibao kipya alichoshirikishwa na K-mode, Mitaa na Sleazo kutoka maeneo ya Kisauni katika kaunti ya mombasa kinachojulikana kwa jina Boom Dem
Monsta ni mhitimu wa shahada ya maswala ya jamii  katika chuo kikuu cha Mt.Kenya tawi la Thika mwaka  wa 2013 .
katika mitandao ya kijamii msanii huyu utampata facebook:monsta monk au barua pepe  simonfuraha4@gmail.com au simon.furaha@yahoo.com





Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: