Friday, 22 September 2017

NAMWAMBA GUMZO MITANDAONI

ad300
Advertisement
Hatimaye aliyekuwa mbunge wa Budalangi Ababu Namwamba amepata kazi ya kuongoza kamati maalumu ya kumfanyia kampeni Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mpya wa Oktoba 26.
Baada ya tume ya uchaguzi kuweka siku mpya kwa uchaguzi wa urais ,ikiwa ni wiki kadhaa kutoka siku mahakama ya upeo chini ya jaji mkuu kubatilisha ushindi wa Rais Uhuru, katika uchaguzi wa Agosti 8 ambapo kati ya majaji wa mahakama ya upeo wanne kati yao walisema uchaguzi haukufikia mahitaji ndipo walipobatilisha uchaguzi huo ambao Uhuru Kenyatta alishjnda kwa asilimia 54 zaidi ya kiongozi wa muungano wa NASA Raila Odinga aliyepata asilimia 45
Hapo jana tarehe 21 mwezi huu Namwamba aliweka picha kwenye mtandao wake wa kijamii wa facebook kuwa amepewa jukumu la kuwa kiongozi wa kamati maalum ya wajumbe 23 kutoka sehemu mbalimbali za Kenya kumfanyia kampeni ya kuchaguliwa tena kwa Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto katika uchaguzi wa Ockota 26 ambako aliahidi kutembea Kenya nzima kufanya kampeni ili Rais na naibu wake wachaguliwe tena .
Katika kamati hiyo inayojulikana  mbele iko sawa kampeni team,  itaongozwa na mwenyekiti Moses Kuria ambaye ni mbuge wa Gatundu Kusini, naye Ababu Namwamba ndiye kiongozi wa kamati hiyo.
Wingine kwenye kamati hiyo ni Nixon Korir,Sabina Chege,Njogu Barua ,Kago wa Lydia ,Martha Wangare,Nelson Koech, Gladys Shollei,Naisula Lesuuda , Beatrice Elachi ,Mishra Kiprop , Racheal Nyamai,Erick Muchangi,Rashid Mohammed , Joyce Lay, Didimus Barasa , Tony Kibangendi , Danson Mungatana , Mwende Mwinzi , Dr David Songok, Parto Munene ,Donya Doris Toto, John Waluke na Ndindi Nyoro.
Namwamba amepewa jukumu hilo baada ya kuhama chama cha ODM na kujiunga na chama cha leba ambapo yeye ndiye mwenyekiti wa chama hicho ambacho kinaunga mkono kuchaguliwa tena Rais
Uhuru Kenyatta  kwa awamu ingine ya miaka mitano.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: