Thursday, 24 January 2019

Chachu ya Radio Salaam yarudi

ad300
Advertisement
Takribani zaidi ya miaka 13 sasa Radio Salaam imekuwa stesheni bora katika mkoa wa Pwani na Kenya kwa ujumla katika maswala mbalimbali kuhusu jamii,siasa na maendeleo.
katika miaka 13 hii Radio Salaam imekuwa namba moja katika kukuza na kutoa wanahabari tajika katika nchi ya Kenya na ulimwengu mzima kama vile Rashid Abdallah naye Lulu Hassan wanaotajika zaidi katika runinga ya citizen huku mwenzake Ali Manzu akipasua anga katika runinga ya KTN bila kuwa sahau wanahabari waliofanya vyema katika tansia hii katika ulingo wa kimataifa kama Ahmed Bahajj aliyekuwa Radio China ambaye kwa sasa amerudi chini nakuendeleza tajriba yake  katika sekta ya michezo katika Runinga ya KTN.
Huku pia katika maswala ya uongozi Radio Salaam imetoa viongozi tajika na pwendwa kwa wanaichi wao kama vile mbunge wa eneo bunge la Nyali Mhe.Mohammed Ali.
Kwa sasa Radio Salaam inapasua anga zake katika kaunti sita za mkoa wa Pwani kupitia mitabendi ya 90.7 huku ikijikita zaidi katika maswala ya mitandao ya kijamiii ya facebook kupitia ukurasa wake wa SALAAM KENYA  na tovuti yake ya www.salaamfm.co.ke ambapo ukitaka kupata habari za kemukemu ukielekea katika kurasa hizo utakuwa wa kwanza kuzipata .
Kando na mitandao ya kijami Radio Salaam imejikita zaidi katika programu za kisasa kwenye simu ambayo inampa fursa msikilizaji,uhuru wakusikiza vipindi mbalimbali kutoka katika simu yake ya mkononi .
kwa sasa radio hii imejaaliwa kuwa na wanahabari walio na tajriba katika tasnia hii wakiongozwa naye mkurungezi wa stasheni bw.Salim A Cheka huku mkuu wa vipindi akiwa Ibrahim Mahmoud nacho kitengo cha masoko kikiongozwa naye Bw.Bwanaobo bin Din .
Vipindi vinavyokuwa hewani kwa sasa vinatikisa anga kwa kuwa na manahodha mahiri kama vile cha Kauli Yako ambapo siasa na maswala mbali mbali yanajadiliwa huku wageni mbali wakialikwa katika kiti moto kwa maswali ya wasikilizaji huku uskani ukishikiliwa naye Omar Aboud nakupewa nguvu za kutosha kutoka kwa Seneta mtagazaji Abuubakar Swabir huku Farashani ukipata dondoo za afya,familia,maswala ya urembo na wanawake bila kusahau kitengo maaluum cha mapishi jikoni kutoka kwake nahodha Mishi Bint Haruni.
Salaam ni nusu ya kuonana hivo basi Salaam mitaani ikiongozwa naye Alamini wa Somo huku jahazi likiendeshwa nao manahodha waledi Mohammed Ali naye Munna Swaleh huku kipindi cha Drive show kilicho na lakabu ya Utepe Drive Show kikiongozwa naye Nahodha Mjukuu wa Muarubaini Real Kajinga akiwa anapewa shavu na dada wa nguvu Menza  huku kipindii cha Siasa cha Kongamano kikiongozwa naye Hajj Kibwanga ambapo utakutana nao watu mbali mbali mashuhuri huku Jukwaa haliezi kuwa Jukwaa bila kuwa huru bila mada nyeti wala mada teule ikiongozwa naye kijana na mwanahabari anayekuwa kwa kasi zaidi katika tasni hii Mohammed hateeb almaaruf Presenter001 maswala ya dini haya kuwachwa nyuma katika Radio Salaam kwani masheikh mbali mbali wakiongozwa naye nahodha wa maswala ya dini Salim Zani
Miezi kadhaa inayokuja katika mwaka huu wa 2019 chachu ile uliyokuwa ukiipata miaka 13 nyuma utaipata huku vipindi vyote vya kijamii kama vile Ambari Kondeni na Ukwasi wa lugha na bila kusahau watakupepurushia matukio yote  makubwa yatakavyojiri hivo basi usipitwe tena kutegea Radio Salaam 90.7 kwani daima dawamu utaangazia ,watakujuza,watakuhabarisha na watakuelimisha .
Bila kusahau kwa habari za utendeti na za uhakika sikiza habari za Radio Salaam kila baada ya jisaa upate zinavyojiri kitaifa na kimataifa.
Hii ni ishara tosha kuwa Radio Salaam ni radio pendwa katika taifa la kenya kwa ujumla basi ukitaka kukuza biashara yako njoo utangaze na Radio Salaam 90.7.
RADIO SALAAM 90.7 INAKUANGAZIA

Share This
Latest
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: