Tuesday, 6 November 2018

Wakaazi wa watamu walalamika kwa mradi kutoendelea

ad300
Advertisement
bango linaloonesha shule ya sekondari ya watamu katika mchoro 
Ni bango lililoko katika barabara ya kuelekea katika kijiji cha kitalii cha Watamu katika eneo bunge la Kilifi Kaskazini katika kaunti ya Kilifi ambapo niliekwa miaka kadhaa sasa eneo hilo likiashiria ujenzi wa shule ya sekondari katika eneo hilo .
Ilikuwa furaha kwa wakaazi wa Watamu ambako alikuwa mbunge wa eneo hilo wakati huo Gideon Mung`aro alikuja kueka jiwe la msingi akiahidi kujenga shule hiyo ambayo ingekuwa historia baada ya miaka 53 ya Uhuru wa taifa hili la Kenya kwani wanafunzi wingi hutoka katika mji huo huenda  kupata elimu katika eneo la Dabaso ,Gede , Malindi au katika maneneo ya mbali ikiwa sababu kuu ni kuwa mji huo hauna shule ya Sekondari ya serekali.
Licha ya kuwa bango hili liko karibu na shule ya msingi ya Watamu ambayo imejaa sifaa lukuki za kutoa wanafunzi wanao faulu katika mitihani yao ya darasa la nane lakini kinaya kikuu ni bango hili ambalo mpka sasa msingi wa shule haujaonekana .
Swali kuu ni je nani amesahau majukumu yake au bango hili liliekwa kwa sababu za kisiasa au je Kaunti ya Kilifi imemsahau huyu mwanafunzi aliyetamani kusoma karibu na nyumbani au serekali kuu kupitia wizara ya elimu ndio ilaumiwe kwa miradi hewa kama hii....
Je mbunge wa sasa wa eneo hili akipita halioni hili bango akawa mkombozi wa kihistoria katika kuikuza elimu ya eneo hili kwa ujumla na pia kuokoa wanafunzi wingi kutokana na kuacha shule mapema pia kumsaidia yule mkaazi wa watamu ambaye hana uwezo kumpa mwanawe nauli ya kila siku kwenda kutafuta elimu kwenye maeneo ya mbali .
Wakaazi wingi waliozungumza nami wanasema wanaimani taarifa hii itawafikia wahusika wakuu na kuhakikisha mradi huu basi utaendelezwa huku wakiwa na imani kuu kwa serekali kuu na ile ya kaunti na mbunge wa eneo hili kuwa watajitokeza na kuwa kifua mbele kuhakikisha shule hii imejengwa kwa viwango vya kisasa na kuhakikisha wanafunzi wa eneo hilo wanapata elimu bora kutoka kwa shule hiyo.


Share This

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

Related Posts

0 comments: