![]() |
Advertisement |
![]() |
Muigizaji Wema Sepetu |
Muigizaji wa tasnia ya filamu nchini Tanzania Wema Sepetu amefungiwa na baraza la sanaa nchini humo kwa kile kinachosemekana kama video isiyo na maadili iliyosambaa sana katika mitandao ya kijamii.
Kwa niaba ya baraza la filamu nchini Tanzania uongozi umeamua kumfungia msanii huyo wa mdaa usiojulikana kuanzia leo ijumaa ya tarehe 26 mwaka 2018 huku wakisisitiza kuwa Wema amekeuka maadili na tamaduni ya mtanzania kwa tabia zake za ajabu haswa katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram.
"Baraza la filamu limemfungia Wema katika shuhuli zake za uigizaji na sanaa kwa mdaa usiojulikana na mpaka pale baraza hili litakapo ridhishwa kuwa amejirekembisha na tabia hii iliyotia aibu taifa" alisema mualikishi wa baraza hilo leo katika kikao na wanadishi wa habari jijini Dar es Salaam. huku akieka wazi kuwa wema atafatiliwa kwa karibu maadili yake na baraza hilo
Adhabu yake imekuja siku chache tu baada ya msanii huyu kuomba msamaha kwa jamii mbele ya vyombo vya habari kutokana na video hiyo.
0 comments: