Advertisement |
Jengo lililoporomoka katika mji wa Malindi |
Mtu mmoja amefariki baada ya jengo lenye ghorofa saba kuporomoka mjini Malindi kwenye kaunti ya Kilifi.
Kulingana na baadhi ya waliofika katika eneo hilo, mkasa huo umetokea mwendo wa saa kumi na moja alfajiri huku kukisikika mlio mkubwa ulioambatana na moshi wa nyumba hiyo ambayo iliwa ingali inajengwa.
Kwa kujibu wa mshirikishi wa shirika la msalaba mwekundu kanda ya pwani Hassan Musa ni kwamba juhudi za ukozi zinaendelea huku watu saba tayari wakiwa wameokolewa.
Aidha Musa amesema kuwa kuna hatari kubwa huenda ikatokea kwa kuwa jumba hilo limeangukia sehemu ya kujaza mafuta huku akiwataka wanachi kuwa na subra.
0 comments: