Advertisement |
kihistoria katika karne hiyo ya 14 Lamu ilikuwa na jamii mbali mbali wakiwemo wareno,wabulushi, wachina na makabila ya wenyeji.
Lamu Fort ni jumba la kihistoria ililojengwa mwaka 1813AD chini ya mfalme wa Pate Sultan Fumo Madi Ibni AbdiBakar, lengo na shabaha ya sultani huyo kujenga ngome hiyo ni kuwalinda watu wa Lamu na wavamizi kama wareno na wengineo ambako mpaka sasa jengo hilo linatumika kama jumba la makumbusho na shuhuli zingine za jamii kama vile harusi.
Kaunti ya Lamu watu wake kwa asilimia 90% ni waislamu ambako ndani yake kuna zaidi ya misikiti 20 bila kusahau msikiti mkongwe msikiti wa Riadha uliojengwa mwaka wa 1900AD na kuhudhuriwa na masheikh mbali mbali kutoka nchi tofauti za ulimwengu waliokuja kufunza dini ya kiislamu .
Miaka ya nyuma Lamu ilikuwa ni soko la kimataifa ambako watu walikuwa wanauza nafaka, mikoko,bidhaa za samaki na vitu vingine katika soko la kimataifa.
Asilimia 85% ya wakazi wa kaunti ya lamu ni wavuvi na wanafanya kazi hii kujikimu kimaisha, kando na uvuvi, utalii ndio uti wa mgongo wa kaunti hii kwa miaka na dahari kwa kuwa na mahoteli ya kifahari ya watalii duniani.
kisiasa kaunti ya Lamu iko na maeneo mawili ya ubunge ambayo ni Lamu magharibi na Lamu mashariki ikiwa chini ya Gavana kama mkuu wa kaunti huku wanawake wakiwakilishwa na muakilishi wa kike nayo seneti ikiwakilishwa na seneta bila kusahau wadi kumi zinazo wakilishwa na waakilishi wa wadi tofauti mtawalia.
Lamu ni kaunti iliyojaa madhari mazuri ya kuvutia sio baharini tu hata bara pia .
Huezi kutaja Lamu bila kusahau kutaja punda kwani ni ndio usafiri pekee ndani ya mji huo wa kiihistoria,punda hutumika kubeba mizigo kutoka kwenye jet ya kuingilia lamu, na pia kama kivutio kikuu cha utalii.
kila mwaka watalii wa kigeni na wale wa ndani hujumuika pamoja katika tamasha tamasha la utamaduni la lamu, ambako mashindano ya kila aina kama vile mbio za punda, kuongelea, mashindano ya mashua hufanyika na usiku wenyeji na wageni hujumuika kwa pamoja kutumbuizwa na wasanii mbalimbali kutoka nchi tofauti barani afrika na ulimwengu kwa ujumla, bila kusahau maonesho mbalimbali ya jamii za kaunti ya lamu.
Safari za anga zinaishia katika uwanja wa ndege wa Manda nazo za barabara zinaishia katika mji wa
Mokowe ambako utapanda boti kukuleta katika kisiwa cha kihistoira cha lamu.
0 comments: