Advertisement |
Seneta Kipchumba Murkomen amemkaribisha Moses Wetangula katika chama cha Jubilee baada ya chama cha ODM kutaka kumpokonya kiti cha uongozi wa wachache katika seneti.
Maseneta wa ODM walimuandika barua spika wa seneti Ken Lusaka wakimshawishi amuondoe Wetangula kwenye kiti hicho na badala yake kipewe seneta wa Siaya James Orengo.
Murkomen alimshawishi Wetangula kuhamia Jubilee ambapo kuna mpangilio dhabiti wa kufanya mambo ikilinganishwa na NASA ambapo hakuna utaratibu wowote. " Nataka kumkaribisha seneta Wetangula katika chama cha Jubilee iwapo amechosha watu katika muungano wa NASA,yuko huru kujiunga nasi hata kabla ya Jumanne ijayo na ninamuhakikishia kwamba nitampea kiti na atajisikia kuwa nyumbani,' Murkomen alisema. " Namhurumia sana kakangu Wetangula kwa yale amefanyiwa, niko tayari kumuweka katika upande wa wengi katika seneti," Murkomen aliongezea. Haya yanajiri baada ya spika wa seneti Ken Lusaka kudhibitisha kuwa alipokea barua kutoka kwa maseneta wa ODM wakimtaka amuondoe Wetangula kwa kiti cha uongozi wa wachache katika bunge na kipewe seneta wa Siaya James Orengo. Maseneta hao walidai kuwa ODM iko na maseneta wengi katika seneti ikilinganisha na chama cha Ford Kenya ambacho kiko na Wetangula pekee na ambaye ni kiongozi wa chama hicho
0 comments: