![]() |
Advertisement |

Duale kwa upande mwingine aliikosoa serikali kwa kuendeleza vita dhidi ya sukari bandia na ya magendo kwa madai kuwa inalenga jamii fulani nchini. Kulingana na Ngunjiri, Duale na Murkomen wamekosa kuipa serikali nguvu kupitia nyadhifa zao serikalini na badala yake kuisaliti.
"Katika nafasi zao kama viongozi wa walio wengi katika mabunge ya kitaifa na seneti, Murkomen na Duale wanatarajiwa kuunga mkono sera na agenda za serikali katika seneti na bunge la kitaifa. Ni wazi kuwa hawawezi. Inawapasa basi kujiuzulu," Alisema Ngunjiri.
Alisema kuwa atamsihi rais kuandaa mkutano wa bunge ili kujadiliana kuhusu kuondolewa kwa wawili hao. "Wasipojiuzulu, nitamuomba kiongozi wa chama kuita mkutano wa wabunge tutakapojadiliana kuhusu nyendo zao kwa nia ya kuwafurusha ofisini," Alisema.
0 comments: