Advertisement |
Licha ya kipaji kikubwa cha muziki, Ali Kiba ni mchezaji soka wa mwenye kipaji cha hali ya juu cha kusakata kabumbu,hata hivyo, mashabiki wa msanii huyo wanajiuliza maswali mengi ikiwa kweli atawaridhisha mashabiki wake wa soka na wale wa muziki kwa wakati moja.
Ali kiba ameanza mazoezi mazito ya kujiandaa kwa michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
kocha wake Juma Mgunda aliyezungumza na mtandao wa Bongo5, Ijumaa, Agosti 3, haikuwa kazi rahisi kupata saini ya mchezaji huyo. “Tumemsajili Ali Kiba kwa kuwa anajua kucheza mpira na sio kwa sababu ni msanii mzuri na anajua kuimba”
kocha Mgunda aliufuatilia mchezo wa Ali Kiba na kushawishika kuwa ni mchezaji mzuri. “Ali ni mchezaji mzuri sana, anajua mpira kama mlivyomuona leo kwenye mazoezi ni mchezaji ambaye ana haki na uwezo wa kuichezea Coastal Union na akaisadia timu” alisema.
0 comments: