![]() |
Advertisement |
Mifereji katika kaunti ya Mombasa na kaunti jirani ya Kilifi imekauka kutoa maji kutokana na uhaba ulioko kwa sasa uliosababishwa na shirika la kusambaza umeme nchini KPLC kukata umeme katika bomba kuu la Baricho kutokana na deni la shillingi millioni 40.
Huduma hii ilikatizwa baada ya bodi ya maji katika mkoa wa Pwani kushindwa kulipa deni hilo kwa shirika hilo la umeme.
Bodi hiyo ya maji Pwani imejitetea kuwa bado haijapokea pesa kutoka kwa hazina kuu ya serekali huku wakisisitiza wako tayari kulipa deni hilo la shirika la umeme inayowadai kampuni ya kusambaza maji katika kaunti ya Kilifi inayodaiwa shillingi Billioni 1 nayo kampuni mwenza katika kaunti ya Mombasa ikidaiwa shillingi Billioni 1.2
Huku wakaazi wa Kaunti ya Kilifi wakizidi kulalama kwa ada ya juu wanayotozwa na kampuni ya maji kila mwezi.
0 comments: