Advertisement |
Raila awaamrisha wafuasi wake kutumia bidhaa na huduma za kampuni ambazo muungano huo ulidai kuwa, kampuni hizo zilikuwa zikishirikiana na Jubilee kuvuruga kura ya Agosti 2017,ametangaza kuondoa marufuku hiyo.
Waziri Mkuu huyo wa zamani amewataka wafuasi wa NASA mara moja kuanza kutumia bidhaa na huduma za Safaricom, Bidco, Brookside, Haco na kampuni zingine ambazo huenda ziliathirika kufuatia amri ya 'ususiaji'.
Raila amesema wakati wa maadhimisho haya siku ya Leba katika uwanja wa Uhuru Park. Kiongozi huyo wa chama cha ODM amesema, makubaliano yake na Rais Uhuru Kenyatta ndio sababu ya kuondoa marufuku hayo ya kiuchumi.
Mnamo Novemba 2017 kinara huyo mkuu wa NASA na vinara wenza waliwaamrisha wafuasi wake kususia bidhaa na huduma za kampuni zilizotajwa.
Ajenda ya 'ususiaji' ilisukumwa mno na wakili Miguna Miguna ambaye alijitangaza kuwa jenerali wa vuguvugu la NASA la National Resistance Movement (NRM).
Haya yalianza baada ya Uhuru kutajwa mshindi wa kura ya urais ya marudio ya Oktoba 26, kura iliyosusiwa na Upinzani. Hata hivyo sio wazi kuhusu ikiwa ususiaji huo uliathiri au la kampuni zilizotajwa na Upinzani NASA.
0 comments: