Advertisement |
Wafugaji hao waliokuwa wameingia Tanzania bila idhini kutafutia ng'ombe wao lishe
Ruto aliwapongeza wafugaji hao kwa kuwa na subira na kuwaahidi kuwa serikali itabuni mbinu kabambe ya kuwepo na bima kwa mifugo Takriban familia 22 kutoka kaunti ya Kajiado sasa zina sababu ya kutabasamu baada ya naibu rais William Ruto kuzifidia mamilioni ya pesa baada ya kupokonywa ng'ombe wao na serikali ya Tanzania
Ruto alipeana hundi ya KSh 53 milioni kwa familia hizo Jumatatu Aprili 2 inafahama kuwa nia ya kuwafidia wafugaji hao ni kuwapa motisha ya kuendelea na ufugaji na kuwawezesha kuishi maisha yao ya kawaida. Akizungumza katika uwanja wa Oltiasika Kusini mwa Kajiado, Ruto alisema kuwa hatua hiyo pia inanuia kuleta uhusiano mzuri kati ya nchi hizi mbili, Kenya na Tanzania. "Serikali ilizihurumia familia zilizopoteza mifugo wao kwa nchi jirani, ni wajibu wetu pia kuhakikisha kuna uhusiano bora kati ya hizi nchi mbili na ndio sababu tumeamua kuwafidia wafugaji wetu," Ruto alisema.
Awali wakenya walighadhabishwa na rais John Magufuli alipowapiga mnada zaidi ya ng'ombe 1000 kwa madai kuwa wafugaji waliingia Tanzania kutafuta lishe bila idhini.
0 comments: