Advertisement |
Mutua alidai kuwa haamini ajenda ya mkutano huo na kumkashifu Kalonzo kwa kutaka kuutumia kujipigia debe katika uchaguzi mkuu wa 2022
Aidha, Kalonzo kwa upande wake naye aliadai kuwa mkutano huo ulinuia kuwaleta viongozi wote wa Ukambani pamoja ili wajadili masuala ya maendeleo Upinzani mkali kati ya kinara mwenza wa muungano wa NASA, Kalonzo Musyoka na Gavana wa Machakos Alfred Mutua ulidhihiririshwa wazi Jumatatu Aprili 2. Kalonzo alihudhuria mkutano uliosimamiwa na seneta wa Machakos, Johnstone Muthama ambao ulinuia kuwaleta pamoja viongozi wote kutoka Ukambani ili wafanye kazi kwa pamoja. Ikizingatiwa kuwa mkutano huo ulikuwa uhudhuriwe na viongozi wote wa Ukambani licha ya tofauti zao za kisiasa, gavana Alfred Mutua alidinda kuhudhuria mkutano huo. " Mkutano huo umekumbwa na masaibu mengi sana, viogozi wanajigamba na hata kutoa makataa ambayo hayastahili, hakuna masuala ya maendeleo au ya kiuchumi yaliojadiliwa ila mkutano huo ulikuwa wa kisiasa tupu ambapo viongozi wengine wanataka kujinufaisha pekee yao, hakuna ajenda iliyozungumziwa kuhusu kuleta jamii ya Wakamba pamoja," Mutua alisema.
" Hebu na sisi viongozi tuheshimiane na tulete jamii ya Wakamba pamoja, tusiwe viongozi wa kujitakia tu ila wa kuwahudumia wananchi vipasavyo," Mutua aliongezea. Kalonzo na Mutua wametangaza azma yao kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao wa 2022.
0 comments: