Advertisement |
Peter John na Martin Mwangi walishtakiwa kwa kutatiza amani na kutishia kumchoma kisu mhudumu wa mkahawa Vincent Mulwa. Waendeshaji mashtaka walisema kisa hicho kilifanyika eneo Makande, Ijumaa, Mei 11.
Kwa kujitetea, Mwangi alisema alijutia kitendo chake na kuongeza kuwa alikuwa mlevi “Sikujua nilichokuwa nikifanya, nilikuwa mlevi, ninaomba mahakama inisamehe ili nirejee nilipe chakula hicho,” alisema.
Wakati wa kisa, mlalamishi alikingwa na wateja wengine wakati wawili hao wakimtishia kumchoma kisu kwa kutaka kupewa pilipili baada ya kuwekewa supu hiyo ya KSh 130.
0 comments: