Thursday, 3 May 2018

UKABILA USIWE KITAMBULISHO CHAKO "RAIS ATAMKA"

ad300
Advertisement
Rais Uhuru Kenyatta alisema kuwa jamii Nzima imesakamwa na siasa za kikabila kwa nusu karne. 
Alisema maridhiano yake na Raila ni mfano wa jinsi tatizo hilo linavyoweza kuangamizwa,kinara huyo wa chama cha Jubilee aliwaomba Wakenya msamaha kwa chochote alichokisema na kuwakera mwaka wa 2017.Rais Uhuru Kenyatta amewataka Wakenya kutotumia kabila zao kwenye mashindano ya siasa ili kuimarisha uthabiti na ustawi wa Kenya. 
Katika hotuba yake kwa taifa siku ya Jumatano, Mei 2, Uhuru alisema kuwa siasa za ukabila zimewaangamiza wengi na kuwataka Wakenya kukoma kutumia makabila yao kama vitambulisho vyao kisiasa, “Tunajivunia utamaduni wetu, lakini isichukuliwe kuwa makabila yetu ndiyo vitambulisho vyetu kisiasa. Tumefanya hivyo kwa nusu ya karne, na nusura ituangamize kabisa.” Uhuru alisema. Kiongozi huyo wa taifa alisema kuwa wengi wametumia ukabila kupata madaraka na kutumia nafasi hizo vibaya ili wasiandamwe na sheria.“Mimi na Raila tuliridhiana, sio kwa sababu tunakubaliana kuhusu kila kitu kwenye siasa na sera, lakini kwa sababu tulikubaliana kuwa Kenya ni yetu sote. “Maridhiano yetu yaliwaalika Wakenya kutambua tena kile walichokijua kwa muda mrefu. Siasa zikiisha, sisi ni wasaidizi wa wenzetu.” Uhuru alisema.
 Rais Kenyatta aliwataka Wakenya na viongozi kuiga maridhiano yake na Raila Odinga ili kuleta umoja, ustawi na maendeleo nchini. Rais Uhuru alimsifu Raila kwa kukubali kuweka ahadi ya maridhiano. “Tulikubaliana kufanya kazi pamoja na kuimarisha umoja wa nchi. Tunatumai kuendeleza na kusisitiza ushirikiano huyo ambao utakuwa na kutofautiana na mashindano.” Uhuru aliongeza. 
Rais Kenyatta aliwataka Wakenya kueneza amani na umoja na kuwataka viongozi kuwasaidia Wakenya kuonyesha umoja na uzalendo kwa njia bora zaidi.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: