Advertisement |
Walichukua mweleko huo baada ya kutofautiana na Raila Odinga kuhusu mkataba wake wa amani na Rais Uhutu Kenyatta.Vyama vya Amani National Congress (ANC) na Ford Kenya vimekamilisha mipango ya kuungana kulingana na katibu mkuu wa chama cha ANC Barack Muluka amesema kuwa vinara hao wawili wa NASA, Moses Wetangula na Musalia Mudavadi wanalenga kuunganisha jamii ya Waluhya kwa kubuni chama kimoja.
Muluka aliongeza kuwa vinara hao walikaribia kutia saini mkataba kama ilivyoripotiwa na gazeti la Standard. “Viongozi hao wawili wanalenga kuunda chama kimoja cha kisiasa chenye mtazamo wa kitaifa kuliunganisha eneo la magharibi na kuungwa mkono na Wakenya wote.” Muluka alisema. Katibu huyo alisema kuwa wana imani wataafikia kuungana kwa vyama hivyo viwili.
“Ni wazo ambalo tumelitafakari na Wetangula na Mudavadi wamelitilia maanani.” Muluka alisema. Msimamo wa Muluka uliungwa mkono na mwenyekiti wa kitaifa wa chama cha ANC Kelvin Lunani aliyeongeza kuwa chama hicho kinaangazia mkataba wa kuungana licha ya baadhi ya wanachama wake kulalamikia hatua hiyo. Viongozi wa Ford Kenya Moses Wetangula na Boni Khalwale na yule wa ANC Musalia Mudavadi waliamua kujitahidi kuiunganisha jamii ya Waluhya eneo la magharibi mwa Kenya kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022. , Mudavadi alipuuzilia mbali waliovitaja vyama vya ANC na Ford Kenya kama vyama vya siasa za maeneo. Alisema vyama hivyo vimewateuwa wataalamu kuendesha shughuli za kuungana na kuwa wamefanya kazi nzuri. Wetangula aliwaomba wakazi wa eneo la magharibi mwa Kenya kuunga mkono mpango huo.
0 comments: