Thursday, 25 January 2018

RAILA KULA KIAPO SAA NNE ASUBUHI

ad300
Advertisement
  Afisa mkuu mtendaji wa muungano wa NASA Norman Magaya amesema kuwa Raila Odinga atakula kiapo Jumanne, Januari 30 shuhuli itakayongozwa na jaji aliyefuzu. 
Hafla hiyo ya kuapishwa kwa Raila imeratibiwa kufanyika saa 4 asubuhi na wafuasi wameombwa kuwasili katika bustani ya Uhuru saa 2 asubuhi. 
NASA imeshikilia kuwa Raila ataapishwa katika bustani ya Uhuru, licha ya gavana wa Nairobi Mike Sonko kusema kuwa bustani hiyo imefungwa kufanyiwa marekebisho.
 NASA imeonekana kuiga matakwa ya katiba yanayotumika kumwapisha rais aliyechaguliwa kihalali,imethibitisha kuwa NASA imepanga kuandaa hafla hiyo katika bustani ya Uhuru jijini Nairobi, licha ya serikali ya kaunti ya Nairobi kutangaza kufungwa kwa bustani hiyo ya kihistoria kwa nia ya kuifanyia marekebisho. Magaya alisema kuwa jaji aliyefuzu anamwapisha Raila kuongoza. “Raila Odinga atakula kiapo saa 4 asubuhi tarehe 30 mwezi huu katika bustani ya Uhuru. Wafuasi wameulizwa kuwa katika bustani hiyo saa 2 asubuhi. Jaji aliyehitimu ataongoza kiapo hicho.” Magaya alisema. 
Magaya alisema kuwa wanatarajia mamilioni ya watu kuhudhuria hafla hiyo. 
Kulingana na jamii ya wafanyibiashara jijini Naiirobi inayoegemea chama cha Jubilee ilizua hali ya mshikemshike ilipotangaza kuwa imehifadhi bustani hiyo kwa shughuli za matibabu siku ya Jumanne, Januari 30.
Gavana wa Nairobi Mike Sonko alitoa ilani iliyotangaza kuwa bustani ya Uhuru itafungwa kwa muda usiojulikana kufanyiwa marekebisho. Serikali pia ilikana ripoti iliyochapishwa kuwa Jumanne, Januari 30 itakuwa siku kuu wakati Raila atakapokula kiapo. Upinzani umepanga kumuapisha Raila Odinga kwa kutumia matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8 waliohesabu wenyewe wakidai kuwa Raila alimshinda Rais Uhuru Kenyatta kwenye uchaguzi huo na kuwa ushindi wa Raila uliibiwa. 
Nia ya NASA ilionekana wakati ilipotishia kumwapisha Raila ikiwa tume ya uchaguzi (IEBC) ingemtangaza Uhuru kuwa mshindi wa marudio ya uchaguzi wa urais wa Oktoba 26. 
Share This

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

Related Posts

0 comments: