Thursday, 1 February 2018

KALONZO YUKO TAYARI KUAPISHWA

ad300
Advertisement
Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka yuko karibu kuapishwa kama Naibu wa Rais wa Wananchi .
Kalonzo hakufika Uhuru Park Jumanne, Januari 30 wakati Raila Odinga aliapishwa 
Walinzi wake waliondolewa muda mfupi kabla ya sherehe hiyo na nyumbani mwake kukavamiwa Kinara wa National Super Alliance (NASA) Kalonzo Musyoka yuko tayari na anataka kuapishwa baada ya kukataa kutokea Jumanne, Januari 30 wakati wa uapisho wa Raila Odinga.
 Wakili Dan Maanzo, ambaye ni rafiki wa karibu Jumatano, Januari 31, alisema "Kalonzo alikuwa tayari kuapishwa pamoja na Raila lakini alizuiliwa kufika uwanjani na maafisa wa polisi". 
 Kulingana na Maanzo, maafisa wa polisi walimzuia Kalonzo katika eneo ambalo hakutaja pamoja na  vinara hao
walikuwa wakikutana ambapo muda uliisha. Mapema siku hiyo,  walinzi wa Kalonzo walikuwa wameondolewa na serikali na kufanya hali kuwa ngumu. Kiongozi huyo wa Wiper alishutumiwa vikali kutoka kwa wafuasi wa NASA na Jubilee ambao walimwita mwoga kwa kudai kuwa aliogopa kufika Uhuru Park na kumwacha Raila Odinga peke yake. Raila aliapishwa peke yake Uhuru Park na kuwaacha wafuasi wa NASA kushangaa sababu za Kalonzo, Musalia na Wetangula kutofika uwanjani.

Watatu hao walitoa taarifa kuelezea kuwa walipatwa na hali ambayo hawakutarajia ambayo ilifanya vigumu kuandamana na Raila Odinga Uhuru Park 
Share This

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

Related Posts

0 comments: