Advertisement |
Ndipo mwenyekiti wa asasi za kiraia katika kaunti ya Lamu Mohammed Abubakar alipotoa ombi kwa niaba yake na wanainchi wa kaunti ya Lamu kwa Rais Uhuru Kenyatta kuwa wanaoimba mrithi wa katibu huyo atoke hapo hapo kaunti hiyo .
katibu huyo alizaliwa katika kaunti ya Lamu alifariki akipokea matibabu baada ya kuvamiwa na wanamgambo wa Al-Shabaab katika eneo la Milihoi katika barabara ya Lamu-Mpeketoni mnamo julai mwaka huu .
Akiongea na wanahabari katika kaunti ya Lamu alimtaja na kumpongeza marehemu Mariam el Maawy kuwa alikuwa mchapakazi ambaye alijitolea kutumikia nchi yake kwa moyo mkunjufu pia alizidi kueleza kuwa kaunti ya Lamu kwenye miaka 50 ya nyuma ilikuwa imeachwa nje kwenye ya maswala ya serekali kuu haswa katika uongozi wa kitaifa.
Aliongezea Abubakar kuwa kaunti hiyo wamepoteza msomi, mama na msahauri mzuri wa jamii ndipo alipomuomba Rais kumchangua mrithi wake ili kuzidii kumtambua na kumpa pongezi daima kwake na kaunti hiyo kwa ujumla .
Usemi huo ulizidi kupata nguvu zaidi pale Gavana wa kaunti hiyo Fahim Twaha na aliyekuwa muakilishi wa wanawake katika kaunti hiyo Shakila Abdallah walizidi kumtaja katibu huyo kuwa msomi na mchapakazi na pia alikuwa kioo cha jamii haswa kwa mtoto wa kike katika kaunti ya Lamu na Kenya kwa ujumla .
0 comments: