Advertisement |
Kinara huyo alisema wamechukua hatua hiyo ya kutoshiriki kwasababu matakwa yao hayajatatuliwa na tume ya uchaguzi ambako wanataka maafisa kadhaa akiwemo afisa mkuu Ezra Chiloba kuondoka ofisini kwani wanasema wao ndio chanzo wa uchaguzi wa Agosti 8 kubadilishwa na mahakama ya upeo .
Seneta huyo alisema maandamano ya leo jumatano yatafanyika huku akiwataka wakaazi wa Nairobi kuwa watakutana katika uga wa Uhuru Park kabla ya kufululiza katika ofisi za IEBC zilizoko katika jumba la Annivesary Towers.
Pia maandamano yatafanyika katika sehemu mbalimbali za Kenya.
Mungano wa NASA walikuwa wameitisha maandamano ya kila siku ya jumatatu na ijumaa ila kwa sasa wameongeza siku ya jumatano kushinikiza matakwa yao kutekelezwa.
0 comments: