Advertisement |
Haya yanajiri siku mbili tu kwenda kwa uchaguzi huo baada ya wajumbe kutoka nchi za Marekani na Uingereza kuwambia Muungano wa Nasa lazima wafate sheria na katiba .
Ndipo Muungano huo ulipojitokeza na kujibu kwa kusema kwa kuwa matakwa yao ya kushiriki uchaguzi mpya wa urais hayakutimizwa basi wao hawatashiriki kivyovyote vile katika uchaguzi huo.
Wajumbe hao pia walisema ni tume ya uchaguzi ya IEBC au Mahakama tu ndio walio na uwezo wa kuhairisha uchaguzi huo.
Nasa wanasisitiza kuwa IEBC hawako tayari kwa marudio hayo ya uchaguzi kulingana na maneno ya aliye kuwa kamishana wake Roselyne Akombe .
"Tulieka wazi kuwa tume ya uchaguzi haiko tayari kuanda uchaguzi huru na haki wa marudio ya urais,hivo basi muungano wa Nasa unaeka wazi kwa kenya,jamii ya kimataifa na wafuasi wake kwa ujumla kuwa uchaguzi wa Oktoba 26 haujafikia matakwa yao na yale masharti ya uamuzi wa mahakama ya upeo hivyo basi wao hawatashiriki."ujumbe kutoka kwa muungano wa Nasa uliosaini
wa na kinara mwenza wa Muungano huo Musalia Mudavadi .
0 comments: