Advertisement |
Kulingana na utafiti uliofanywa na jarida la International journal of obesity ni kuwa watoto wadogo zaidi ya 12,000 nchini Uingereza kuwa wako na unene wa kupindukia kwani karibia wote wako na runinga kwenye vyumba vyao vya kulala wakiwa na umri wa maiaka saba.
Wasichana asilimia 30 walio na umri huo wako na uwezekano kupata uzito wa mwili wa kupindukia wanapofika umri wa 11.
Wakilinganishwa na wenzao ambao hawana televisheni kwenye vyumba vyao vya kulala,
huku watoto wa kiume wakiwa asilimia 20 ya uwezekano wa kupata uzito wa kupindukia.
Watafiti walibaini kuwa watoto wasichana kadri wanavyokaa muda mrefu pia kula ovyo ovyo wakitazama runinga ndivyo wanavyokuwa na uwezakano mkubwa wa uzito wao wa mwili kuongezeka.
Lakini bado hawajapata uhakika wa uhusiano kati ya kutazama televisheni na kuongezeka kwa mwili wa mtoto.
0 comments: