Advertisement |
Uchaguzi wa mbunge wa Lamu Magharibi Stanley Muthama umefutiliwa mbali na mahakama kuu ya Malindi, mbunge huyo wa chama cha Maendeleo Chap Chap alijizolea kura 11,090 dhidi ya kura 10,950 za mpinzani wake wa karibu wa chama cha ODM Rishad Amana, kwenye uchaguzi ambao mahakama imesema ulikumbwa na dosari nyingi
Kulingana na Jaji Weldon Korir alitaka tume ya uchaguzi ya IEBC pamoja na mkuu wa uchaguzi wa eneo hilo kumlipa mlalamishi kima cha shillilngi millioni 3.
Wakati mahakama ilipotoa amri wa kura hizo kuhesabiwa upya, Stanley alisema" ushindi wangu sio wa bahati mbaya na nawaomba wafuasi wangu wawe na subra kwani yeye ndio aliye teuliwa na watu wa lamu magharibi "uamuzi wa mahakama ya Malindi unakuja siku moja tu baada ya mahakama kubatilisha ushindi wa gavana wa Homabay Cyprian Awiti
0 comments: