Advertisement |
Mahakama ya Juu imesema maafisa wa wakuu wa polisi huenda wakawajibika ikiwa wakikosa kumwasilisha Miguna Miguna kortini.
Jaji wa Mahakama ya Juu Luka Kimaru amemwambia Inspekta Mkuu wa Polisi Joseph Boinnet na mkuu wa kitengo cha Ujasusi George Kinoti kuhakikisha Miguna anafika kortini Jumanne, Februari 6.
Miguna alikamatwa Ijumaa, Februari 2 kwa kosa la kujitangaza jenerali wakundi NRM ambalo serikali imesema ni haramu
Amekuwa akizuiliwa katika kituo cha polisi cha Lari tangu Ijumaa hata baada ya amri ya korti aachiliwe kwa dhamana.
Mahakama ya Juu imetaka polisi kumwasilisha kortini jenerali wa Vuguvugu la Kitaifa la (NRM) Miguna Miguna, ama wawajibikie kosa la kutoheshimu korti ikiwa watakosa kufanya hivyo. Polisi wamekwenda kinyume na amri ya korti, ya Ijumaa, Februari 2, iliyotaka Miguna kuachiliwa kwa dhamana ya KSh50,000 pesa taslimu Miguna alikamatwa Ijumaa, Februari 2 na hii ni baada ya polisi kuvunja na kuingia nyumbani kwake na kumpeleka katika kituo cha polisi cha Githunguri na hatimaye kuahimishiwa Lari
Wakili wa Miguna, Edwin Sifuna, mapema alikuwa amedai kwamba polisi walikataa kumruhusu kumwona mteja wake, licha ya mteja huyo kuugua pumu. Miguna alikamatwa siku chache baada ya Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i, kuamrisha kuanza kukamatwa kwa waliohusika na kiapo tata cha Raila Odinga, Jumanne, Januari 30 Miguna ndiye aliyetia saini kwenye cheti cha kumtangaza Raila kuwa Rais wa Wananchi, hafla iliyokosa kuhudhuriwa na vinara wengine wa NASA. Kufuatia kiapo hicho, waziri Matiang’i alitangaza Vuguvugu la Kitaifa la Ukaidi (NRM) kuwa “kundi haramu” kwa mujibu wa kifungu cha Katiba kuhusu Kuzuia Uhalifu wa Kupangwa.
0 comments: