Thursday, 24 January 2019

Chachu ya Radio Salaam yarudi

Takribani zaidi ya miaka 13 sasa Radio Salaam imekuwa stesheni bora katika mkoa wa Pwani na Kenya kwa ujumla katika maswala mbalimbali kuhusu jamii,siasa na maendeleo.
katika miaka 13 hii Radio Salaam imekuwa namba moja katika kukuza na kutoa wanahabari tajika katika nchi ya Kenya na ulimwengu mzima kama vile Rashid Abdallah naye Lulu Hassan wanaotajika zaidi katika runinga ya citizen huku mwenzake Ali Manzu akipasua anga katika runinga ya KTN bila kuwa sahau wanahabari waliofanya vyema katika tansia hii katika ulingo wa kimataifa kama Ahmed Bahajj aliyekuwa Radio China ambaye kwa sasa amerudi chini nakuendeleza tajriba yake  katika sekta ya michezo katika Runinga ya KTN.
Huku pia katika maswala ya uongozi Radio Salaam imetoa viongozi tajika na pwendwa kwa wanaichi wao kama vile mbunge wa eneo bunge la Nyali Mhe.Mohammed Ali.
Kwa sasa Radio Salaam inapasua anga zake katika kaunti sita za mkoa wa Pwani kupitia mitabendi ya 90.7 huku ikijikita zaidi katika maswala ya mitandao ya kijamiii ya facebook kupitia ukurasa wake wa SALAAM KENYA  na tovuti yake ya www.salaamfm.co.ke ambapo ukitaka kupata habari za kemukemu ukielekea katika kurasa hizo utakuwa wa kwanza kuzipata .
Kando na mitandao ya kijami Radio Salaam imejikita zaidi katika programu za kisasa kwenye simu ambayo inampa fursa msikilizaji,uhuru wakusikiza vipindi mbalimbali kutoka katika simu yake ya mkononi .
kwa sasa radio hii imejaaliwa kuwa na wanahabari walio na tajriba katika tasnia hii wakiongozwa naye mkurungezi wa stasheni bw.Salim A Cheka huku mkuu wa vipindi akiwa Ibrahim Mahmoud nacho kitengo cha masoko kikiongozwa naye Bw.Bwanaobo bin Din .
Vipindi vinavyokuwa hewani kwa sasa vinatikisa anga kwa kuwa na manahodha mahiri kama vile cha Kauli Yako ambapo siasa na maswala mbali mbali yanajadiliwa huku wageni mbali wakialikwa katika kiti moto kwa maswali ya wasikilizaji huku uskani ukishikiliwa naye Omar Aboud nakupewa nguvu za kutosha kutoka kwa Seneta mtagazaji Abuubakar Swabir huku Farashani ukipata dondoo za afya,familia,maswala ya urembo na wanawake bila kusahau kitengo maaluum cha mapishi jikoni kutoka kwake nahodha Mishi Bint Haruni.
Salaam ni nusu ya kuonana hivo basi Salaam mitaani ikiongozwa naye Alamini wa Somo huku jahazi likiendeshwa nao manahodha waledi Mohammed Ali naye Munna Swaleh huku kipindi cha Drive show kilicho na lakabu ya Utepe Drive Show kikiongozwa naye Nahodha Mjukuu wa Muarubaini Real Kajinga akiwa anapewa shavu na dada wa nguvu Menza  huku kipindii cha Siasa cha Kongamano kikiongozwa naye Hajj Kibwanga ambapo utakutana nao watu mbali mbali mashuhuri huku Jukwaa haliezi kuwa Jukwaa bila kuwa huru bila mada nyeti wala mada teule ikiongozwa naye kijana na mwanahabari anayekuwa kwa kasi zaidi katika tasni hii Mohammed hateeb almaaruf Presenter001 maswala ya dini haya kuwachwa nyuma katika Radio Salaam kwani masheikh mbali mbali wakiongozwa naye nahodha wa maswala ya dini Salim Zani
Miezi kadhaa inayokuja katika mwaka huu wa 2019 chachu ile uliyokuwa ukiipata miaka 13 nyuma utaipata huku vipindi vyote vya kijamii kama vile Ambari Kondeni na Ukwasi wa lugha na bila kusahau watakupepurushia matukio yote  makubwa yatakavyojiri hivo basi usipitwe tena kutegea Radio Salaam 90.7 kwani daima dawamu utaangazia ,watakujuza,watakuhabarisha na watakuelimisha .
Bila kusahau kwa habari za utendeti na za uhakika sikiza habari za Radio Salaam kila baada ya jisaa upate zinavyojiri kitaifa na kimataifa.
Hii ni ishara tosha kuwa Radio Salaam ni radio pendwa katika taifa la kenya kwa ujumla basi ukitaka kukuza biashara yako njoo utangaze na Radio Salaam 90.7.
RADIO SALAAM 90.7 INAKUANGAZIA

Sunday, 25 November 2018

Barua ya wazi kwa Rais Uhuru Kenyatta


Rais Uhuru akihutubia wakati moja.
MOHAMMED HATIB ABDALLAH
|| Email: muhammadabdallah944@gmail.com

25th November, 2018

Kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya
Uhuru Muigai Kenyatta,

S.L.P - 80100,
Ikulu ya Nairobi,

Mtukufu Rais,

                               MINT: MKOMBOZI WA WALALA HOI KENYA

Rais, Natumai ubuheri wa afya kwa sasa hapo ulipo.
Baada ya kukuona uko mchangamfu katika hafla kadhaa ulipozuru eneo hili la kaunti ya Mombasa ukiwa bega kwa bega na Gavana wa Kaunti ya Mombasa na magavana wengine wa kaunti za hapa mkoani Pwani katika kuanzisha na kufungua miradi kadhaa itakayo wanufanisha wakaazi wa mkoa wa Pwani na Kenya kwa ujumla.
Lakini leo Bwana Rais kwa niaba ya wakenya walalahoi nimeamua kukuandikia waraka huu kukuomba uyatilie mkazo maswala haya kwa niaba ya wakenya wa tabaka la chini.
La kwanza nililolipa kipao mbele ni swala la reli ya kisasa ya SGR kwa sababu wakenya wengi wamepoteza ajira baada ya shirika la reli nchini kuanzisha safari za kubeba makasha kutoka bandari za Mombasa.,wakenya waliokuwa wakitegemea kubeba makasha hayo kupitia malori yao wingi sasa wamebaki wakilia hali huku uchumi mzito ukizidi kuwalemea .
Ulipofungua mradi wa SGR wakenya wengi walifurahia lakini athari zake sasa zimeanza kujitokeza sio kwa madereva tu bali hata kwa wenye mahoteli na wenye vyumba vya wageni katika barabara kuu ya Mombasa Nairobi bila kuwasahau wafanya biashara wanaofanya biashara kando kando na barabara hii .
Rais ombi langu kwa niaba ya wakenya kwako kupitia kwa shirika la reli nchini na kwa waziri wa uchukuzi wapunguze au wagawiyane makasha na madereva wa malori ili hali ya maisha yao na ya hawa wanabiashara irudi kama mwanzo.
Pili Rais ni swala la mnyonge azidi kuwa mnyonge kwa mzigo wa serikali , ni hivi majuzi tu wabunge na maseneta walieka tofauti zao za vyama na wakaja pamoja na kuungana mkono kupitisha mswaada wa nyongeza za mishahara na marupurupu huku wakenya wakawaida wakizidi kuemezewa mzigo huu.
Rais kumbuka kiongozi bora hujulikana wakati wa matatizo na shida kwa heshima na taadhima Rais simama imara katika kumkomboa mkenya huyu mlalahoi kutoka kwa midomo ya viongozi wasio na utu wala huruma kwa wakenya hivyo basi ifikiapo tarehe 27 mwezi Novemba mwaka 2018 usitie sahii mswaada huu kwani wakenya watazidi kuwa katika hali ngumu kimaisha na kiuchumi .
Kumalizia Rais ni swala la Blue Economy ulipofungua warsha juzi katika hoteli ya pride inn katika kaunti za Mombasa ambayo ilileta pamoja magavana wote wa kaunti zote sita za pwani wapwani tulifurahia na kupokea mradi huu kwa mikono miwili kikunjufu huku tukitarajia mengi mazuri kutoka kwa mradi huu, ombi langu kwako mtukufu Rais ni kuwa mradi huu unufaishe wakenya wa tabaka la chini wala sio wale watabaka la walio wachache nchini. Ni mradi najua utakao zalisha ajira hivyo basi kama katika katiba yetu ya Kenya naomba zile asilimia zilizotengwa ziwanufaishe watu wa eneo husika wala isiwe kama swala la Bandari kuwa na wingi wa wafanyakazi kutoka eneo flani au mradi ule wa Base Titanium ambapo umeawacha wakaazi wa kaunti ya Kwale wakilia ngoa nao.
Kukuandikia barua sio kukukejeli wala kukukosoa lakini fahamu anayekwambia uendako kuna shimo hakunyimi safari ila anakujali.
Nina mengi ya kukueleza lakini mdaa haunirusu kumbuka Kenya ni jina nchi ni sisi wanainchi .
Jina langu ni Mohammed Hatib mwandishi wa habari katika stesheni ya Radio Salaam Mombasa,
Shukrani.
 

Tuesday, 6 November 2018

KEN REL BIS Y254 TV HOST WHO IS GIVING WILLY M TUVA AND JAMAL GADDAFI SLEEPLESS NIGHTS

Ken Rel Bis Y254 Presenter
When you speak of Kenyan top Swahili presenters on the entertainment scene Mzazi willy M Tuva, Mwende Macharia, Clemmo CMC and Mwinyi Kazungu will definitely come first on your mind as they are well known for their musical shows on your favourite radio stations Kenya.
Mzazi Willy M Tuva has taken the industry a notch higher by hosting a Swahili musical show on TV and has for years enjoyed monopoly on mainstream media.
Ken Rel Bis with Dj Tiesqa 
Later on KTN unleashed a Talented Swahili presenter who people believed will give Tuva sleepless nights but as time went by he seemed not to stand up to the task.
Now Kenya has a new fresh talent from Y254 TV, youth channel viewed by a huge audience every Monday from 7:30pm- 9:30pm hungry to see the new kid on block, Ken Rel Bis AKA Mr. Exclusives entertaining them with his Swahili Prowess and captivating interviews. Ken Rel Bis asks your favourite celebrities the rarest and unexpected questions that no presenter has had the courage to ask.
Ymashariki also provides celebrity backgrounds and exclusive interviews by reporters such as Meena Ally all the way from Tanzania.
Ken Rel Bis with J.I from Tanzania 
Ken Rel Bis has been in the game for only less than a year but has managed to keep Kenyans glued to screens and garnered lots of praises from fans on social media.
Will he be the next presenter in Kenya come next year. If you don’t think so, check out the interviews he has done with the artistes below.
CMB PREZZO
PRINCESS LEO
DAVID WONDER
J.I FROM TANZANIA
KENDI
JAY MADINI
CHILUBA
VIC MASS LU DOLLAR
RED PEN
MASAUTI
ENOCH BELLA FROM TANZANIA
Just to mention a few.

Ken Rel Bis with CMB Prezzo 

 For more awesome interviews from Mr. Exclusive, have a look at the Y mashariki show on YouTube. And for gossips, remember to watch ChitChat.

Wakaazi wa watamu walalamika kwa mradi kutoendelea

bango linaloonesha shule ya sekondari ya watamu katika mchoro 
Ni bango lililoko katika barabara ya kuelekea katika kijiji cha kitalii cha Watamu katika eneo bunge la Kilifi Kaskazini katika kaunti ya Kilifi ambapo niliekwa miaka kadhaa sasa eneo hilo likiashiria ujenzi wa shule ya sekondari katika eneo hilo .
Ilikuwa furaha kwa wakaazi wa Watamu ambako alikuwa mbunge wa eneo hilo wakati huo Gideon Mung`aro alikuja kueka jiwe la msingi akiahidi kujenga shule hiyo ambayo ingekuwa historia baada ya miaka 53 ya Uhuru wa taifa hili la Kenya kwani wanafunzi wingi hutoka katika mji huo huenda  kupata elimu katika eneo la Dabaso ,Gede , Malindi au katika maneneo ya mbali ikiwa sababu kuu ni kuwa mji huo hauna shule ya Sekondari ya serekali.
Licha ya kuwa bango hili liko karibu na shule ya msingi ya Watamu ambayo imejaa sifaa lukuki za kutoa wanafunzi wanao faulu katika mitihani yao ya darasa la nane lakini kinaya kikuu ni bango hili ambalo mpka sasa msingi wa shule haujaonekana .
Swali kuu ni je nani amesahau majukumu yake au bango hili liliekwa kwa sababu za kisiasa au je Kaunti ya Kilifi imemsahau huyu mwanafunzi aliyetamani kusoma karibu na nyumbani au serekali kuu kupitia wizara ya elimu ndio ilaumiwe kwa miradi hewa kama hii....
Je mbunge wa sasa wa eneo hili akipita halioni hili bango akawa mkombozi wa kihistoria katika kuikuza elimu ya eneo hili kwa ujumla na pia kuokoa wanafunzi wingi kutokana na kuacha shule mapema pia kumsaidia yule mkaazi wa watamu ambaye hana uwezo kumpa mwanawe nauli ya kila siku kwenda kutafuta elimu kwenye maeneo ya mbali .
Wakaazi wingi waliozungumza nami wanasema wanaimani taarifa hii itawafikia wahusika wakuu na kuhakikisha mradi huu basi utaendelezwa huku wakiwa na imani kuu kwa serekali kuu na ile ya kaunti na mbunge wa eneo hili kuwa watajitokeza na kuwa kifua mbele kuhakikisha shule hii imejengwa kwa viwango vya kisasa na kuhakikisha wanafunzi wa eneo hilo wanapata elimu bora kutoka kwa shule hiyo.


Friday, 26 October 2018

Wema afungiwa kuigiza Tanzania

Muigizaji Wema Sepetu 

Muigizaji wa tasnia ya filamu nchini Tanzania Wema Sepetu amefungiwa na baraza la sanaa nchini humo kwa kile kinachosemekana kama video isiyo na maadili iliyosambaa sana katika mitandao ya kijamii.

Kwa niaba ya baraza la filamu nchini Tanzania uongozi umeamua kumfungia msanii huyo wa mdaa usiojulikana kuanzia leo ijumaa ya tarehe 26 mwaka 2018 huku wakisisitiza kuwa Wema amekeuka maadili na tamaduni ya  mtanzania kwa tabia zake za ajabu haswa katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram.
"Baraza la filamu limemfungia Wema katika shuhuli zake za uigizaji na sanaa kwa mdaa usiojulikana na mpaka pale baraza hili litakapo ridhishwa kuwa amejirekembisha na tabia hii iliyotia aibu taifa" alisema mualikishi wa baraza hilo leo katika kikao na wanadishi wa habari jijini Dar es Salaam. huku akieka wazi kuwa wema atafatiliwa kwa karibu maadili yake na baraza hilo
Adhabu yake imekuja siku chache tu baada ya msanii huyu kuomba msamaha kwa jamii mbele ya vyombo vya habari kutokana na video hiyo.




Jengo la poromoka Malindi

Jengo lililoporomoka katika mji wa Malindi 
Mtu mmoja amefariki baada ya jengo lenye ghorofa saba kuporomoka mjini Malindi kwenye kaunti ya Kilifi.
Kulingana na baadhi ya waliofika katika eneo hilo, mkasa huo umetokea mwendo wa saa kumi na moja alfajiri huku kukisikika mlio mkubwa ulioambatana na moshi wa nyumba hiyo ambayo iliwa ingali inajengwa.
Kwa kujibu wa mshirikishi wa shirika la msalaba mwekundu kanda ya pwani Hassan Musa ni kwamba juhudi za ukozi zinaendelea huku watu saba tayari wakiwa wameokolewa.
Aidha Musa amesema kuwa kuna hatari kubwa huenda ikatokea kwa kuwa jumba hilo limeangukia sehemu ya kujaza mafuta huku akiwataka wanachi kuwa na subra.
Kwa upande wake waziri wa afya kaunti ya Kilifi Daktari Anisa Mohamed amesema walioathrika kwa sasa wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali kuu ya kaunti ndogo ya Malindi

Monday, 6 August 2018

Mwanamke ashindwa kulipa bili ya hospitali

Mwanamke mmoja ameshindwa kulipia bili ya hospitali ya kata ya mariakani katika kaunti ya kilifi,mwanamke huyo alilazwa hospitalini mnamo Juni 25 kupitia usaidizi wa Mbunge wa Kaloleni Paul Katana ,Mbunge huyo alilipa KSh 10,000 lakini mgonjwa anatarajiwa kulipa KSh 9,700 za ziada. Mwanamke huyo anazuiliwa kwa zaidi ya wiki ya nne sasa katika hospitali ya kata ya Mariakani, Kaloleni, Mwenda Karisa anaaminika kulazwa katika kituo hicho cha afya kupitia usaidizi wa Mbunge wa Kaloleni Paul Katana aliyeenda kimya baada ya kumlipia kiasi hicho.
Mgonjwa huyo anaugua maradhi ya saratani ya njia ya uzazi na angestahili kuondoka hospitalini humo siku ya  Ijumaa, Julai 20 kama angekuwa amelipa kikamilifu salio. “Tunamsubiri mumewe au mbunge aliyemleta hapa kuja kulipa bili hiyo. Hatuwezi kumruhusu kuondoka pasipo idhini kutoka kwa wakuu wetu,” duru kutoka hospitali hiyo zilisema. Mgonjwa huyo, kulingana na duru hospitalini humo vilevile alikuwa na tatizo sugu la upungufu wa damu, hospitali hiyo haikuwa na damu inayolandana ya kumweka. Baadaye alifanyiwa upasuaji.
Kulingana na Karisa Kahindi, mumewe mwanamke huyo yuko tayari kumsaidia lakini changamoto za kiuchumi zimemlemea. “Niko radhi kusaidia lakini kutokana na changamoto za kifedha na kwamba nina mke wa pili na watoto kadha, siwezi,” alisema. Isitoshe, mume huyo alisema kabla ya mkewe kulazwa hospitalini, hakufahamishwa kwa sababu mwanamke huyo alikuwa akiishi na wazazi wake hadi kufikia sasa. Juhudi za kumfikia mbunge ili kusikia upande wake ziliambulia patupu huku msaidizi wake akisema hajakuwa akijihisi vyema kwa juma moja.