Advertisement |
Mudavadi ambaye ni mkuu wa kampeni za Nasa amewaomba wanainchi kupuuza barua hiyo kwenye mitandao ya kijamii akisema ni porojo tu hizo.
kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi akihutubia mkutano uliopita . |
"kuna barua ghushi inayoeneza fununu kwenye mitandao kuwa nimehama Nasa , huo ni uongo mtupu niko Nasa kudumu sitagura kamwe ".Alisema hayo alipokuwa akiwahutubia waandishi wa habari katika ofisi za okoa kenya zilizo jijini Nairobi.
Alisisitiza kuwa jamii lazima ielewe kwenye mitandao hiyo kuna sarakasi nyingi hivo watu wasipende kuamini mambo kama hayo kwani ni fununu tu yeye yuko Nasa kudumu.
Alipokuwa akiongea hayo alikuwa ameandamana na seneta wa Bungoma Moses Wetangula aliye kiongozi wa Ford Kenya na seneta wa Siaya James Orengo.
Barua hii imekuja siku kadhaa tu baada ya aliyekuwa kinara mwenza kwenye muungano wa Nasa na pia alikuwa gavana wa Bomet Isaac Ruto wa chama cha mashinani (CCM) kugura muungano huo na kutangaza kumuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee katika uchaguzi unao kuja wa Oktoba 17 baada ya mahakama ya upeo inayoongozwa na jaji mkuu David Maraga kufutilia mbali uchaguzi wa Agosti 8.
0 comments: