Wednesday, 20 December 2017

KIAMBU NA KILIFI ZAZUA HISIA

ad300
Advertisement

Kaunti za Kiambu na Kilifi zimezidi kuzua hisia mseto kwa watu mbali mbali kuhusiana na hoja ya mabunge yao kutaka kupitisha mswaada wa kutoa asilimia sabini ya nafasi za kazi katika taasisi za umma na zile za kibinafsi kwa wenyeji pekee.
Hatua hii imepingwa vikali na tume ya utengamano na kutajwa hatua hii kama ubaguzi ambao ni kinyume na katiba. Mwenyekiti wa NCIC Francis  Ole Kaparo ametishia kwenda mahakamani kupinga hatua ya kaunti hizi mbili iwapo watapitisha mswaada Huu kuwa sheria kwenye kaunti zao.
Hatua ya kaunti hizi huenda ikazua ukabila na kuvuruga umoja na utengamano nchini.
Je mkenya maoni yako ni yapi kuhusu hatua ya kaunti za kiambu na kilifi?
Je waona italeta ukabila au ni hatua ya kukabiliana na ukosefu wa ajira haswa katika kaunti zetu?

Share This

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

Related Posts

0 comments: