Tuesday, 9 January 2018

WANAWAKE SAUDIA KUANGALIA MPIRA SASA

ad300
Advertisement
Wanawake wanaoishi katika ufamle wa kiarabu wa saudia wataruhusiwa kuanzia mwezi huu kuhudhuria kwenye michezo ya kandanda ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya ufamle huo. 
Maafisa wa taifa hilo wamesema kuwa mashabiki wa kandanda wanawake wataanza kuingia katika viwanja vya mpira kuangalia michezo mitatu inayohusisha timu zinazoshiriki ligi ya nchi hiyo katika mechi ya Ijumaa, Jumamosi na januari 18 mwaka huu .
October 2017, idara inayohusika na masuala ya michezo ya Saudi Arabia ilitangaza kufikia 2018 viwanja vitatu ambavyo vilikuwa vinatumika na wanaume tu vitaandaliwa kwa ajili ya kutumiwa pia na wanawake ikiwa ni pamoja na kuwa na maeneo maalumu ya kukaa.
Mwana wa Mfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman  ameondoa marufuku ya wanawake kujihusisha na mchezo wa kandanda, wakati akijaribu kurudisha heshima ya nchi hiyo kimataifa kuhusiana na haki za mwanamke katika nchi hiyo.
Share This

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

Related Posts

0 comments: