Tuesday, 9 January 2018

LOWASSA AKUTANA NA RAIS MAGUFULI

ad300
Advertisement
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli leo amekutana na waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa Ikulu Dar el Salaam.
Lowassa amempongeza Rais Magufuli kwa maendeleo anayofanya kwa sasa Tanzania akitaja maendeleo kama ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha umeme katika maporomoko ya mto Rufiji,Elimu bila malipo,Viwanda na Reli ya kisasa standard gauge, viwanda ambavyo vitazalisha ajira kwa watanzania walio wengi ambao hawana ajira .

"Nimepata faraja kuja ikulu kuonana na rais tumezungumza na kumpongeza kwa kazi nzuri anayoifanya ,ni lazima tukiri anafanya kazi nzuri na anahitaji kutiwa moyo". lowassa alisema

kwa upande wa Rais Magufuli alisema Lowassa ni mwanasiasa mzuri.
"Mhe Lowassa ameniomba mara nyingi nikutane naye na leo nimekutana nae tumezungumza mambo mengi ameniambia ya kwake na mimi nimemwambia ya kwangu"
Rais Magufuli pia alitoa wasaa kwa jamii kwa ujumla kuwa waendele kuwaenzi wanasiasa wazee kama lowassa na wengine  ambao kwa nyakati fulani walifanya mambo mazuri kwa taifa hili.
Share This

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

Related Posts

0 comments: